Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amneonya kwamba jaribio lolote la kupanua mipaka inayoshikiliwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga nchini Ukraine , hazitakubalika na kuiambia Urusi kuondoa vifaa 1,000 vya kijeshi kutoka katika ardhi ya nchi jirani ya Ukraine.
Akizungumza baada ya mkutano na waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi , katibu mkuu wa NATO ameeleza matumaini ya tahadhari juu ya matarajio ya makubaliano tete ya kusitisha mapigano kati ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi na majeshi ya Ukraine.
O-Ton Stoltenberg
Matamshi ya Stoltenburg yanakuja wakati jeshi la Ukraine limetangaza kuanza kuondoa silaha kali kutoka katika mstari wa mbele wa mapambano.
Nahuko Ugiriki mpango wa utatuzi wa matatizo ya uchumi wa Ugiriki unaotarajiwa kurefushwa kwa miezi minne unatazamiwa kupata uungwaji mkubwa mkono katika bunge la Ujerumani baada ya idadi kubwa ya wabunge katika chama cha kihafidhina cha kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuonesha ishara ya kuunga mkono.
Bunge litapiga kura Ijumaa katika makubaliano yaliyofikiwa na mawaziri wa fedha wa mataifa wanachama wa sarafu ya euro. Volker Kauder, kiongozi wa wabunge wa chama cha kansela Merkel , amesema wengi wa wabunge wa chama hicho wataunga mkono makubaliano hayo.
Muungano wa vyama vinavyounda serikali inayoongozwa na chama cha kansela Merkel ikiwa ni pamoja na chama cha siasa za wastani za mrengo wa shoto cha Social Democratic SPD, chama ambacho kinaunga mkono kwa dhati mapendekezo hayo, una jumla ya robo tatu ya viti bungeni.
Wakati huo huo Wabunge nchini Uholanzi wamepiga kura leo kuunga mkono urefushaji kwa miezi minne mpango wa uokozi wa uchumi wa Ugiriki.